Israel yalaani matamshi ya afisa wa Ulaya kuhusu ‘mauaji ya kimbari’ Gaza


Israel siku ya Alhamisi imekosoa vikali matamshi ya Makamu wa Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Teresa Ribera, ikiita vita vya Gaza kuwa ni “mauaji ya halaiki,” ikimtuhumu kuwa “msemaji wa propaganda za Hamas.”
“Tunalaani vikali madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na Makamu wa Rais Mtendaji wa Tume ya Ulaya,” ameandika Oren Marmorstein, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, kwenye mtandao wa kijamii X.
“Badala ya kutetea shutuma za ‘mauaji ya kimbari’ yanayoenezwa na Hamas, Ribera alipaswa kutoa wito wa kuachiliwa kwa mateka wote na Hamas kuweka silaha chini ili kumaliza vita.”
Wakati huo huo Jeshi la Israel limebainisha kuwa linaudhibiti wa kijeshi wa asilimia 40 ya Mji wa Gaza, kwa mujibu wa msemaji wake Brigedia Jenerali. Effie Defrin, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Septemba 4, 2025.
Comments are closed.