Uganda: Kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Kizza Besigye yaahirishwa hadi Oktoba 1

151
kwibuka31

Nchini Uganda, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, Kizza Besigye, hakuhudhuria ufunguzi wa kesi yake ya uhaini siku ya Jumatatu asubuhi Septemba 1, katika Mahakama Kuu ya Kampala.

Akiwa amezuiliwa tangu kukamatwa kwake nchini Kenya mwezi Novemba mwaka jana, mmoja wa mawakili wake amedai kuwa mteja wake alikuwa akisusia kusikilizwa kwa kesi hiyo. Mnamo Agosti, upande wa utetezi ulidai kuwa jaji anayesimamia kesi hiyo alikuwa na upendeleo, haswa baada ya kukataa kumpa mshtakiwa dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 1.

Mahakama ilijiridhisha kuwa wadhamini walikuwa watu sahihi na kwamba walikidhi vigezo vilivyotakiwa. Lakini Jaji Rosette Comfort Kania alikataa kuwaachilia kwa dhamana wawili hao akitaja uzito wa mashtaka na hasa kutokana na kuendelea kwa uchunguzi.

‘‘Uhalifu huu unadaiwa kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini Uganda na mataifa mengine, kwa hiyo itachukuwa muda kukamilisha uchunguzi ambavyo ni tofauti na uhalifu ambao umefanyika Uganda pekee’’, Jaji Kania alisema katika maamuzi yake yaliyosomwa na msajili Ssalmu Ngoobi.

Kulingana na upande wa mashtaka, Dkt. Besigye, Hajj Lutale, Kapteni Denis Oola, na wengine ambao hawajulikani waliko wanadaiwa kupanga njama ya kupindua serikali kwa kutumia silaha kati ya 2023 na Novemba 2024.

Njama hiyo inadaiwa kupangwa katika nchi kadhaa ikiwemo Uswizi, Ugiriki, Kenya na Uganda.

(Muhirwa Innocent /Indorerwamo.com)

Comments are closed.