DRC: Rais Tshisekedi amtaka Kagame kuacha kuwaunga mkono waasi

312
kwibuka31

Rais wa DRC Felix Tshisekedi akizungumza akiwa jijini Brussels Ubelgiji amemtaka mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kuacha kuwasaidia waasi mashariki ya DRC na kutengeneza amani.

Kauli ya Tshisekedi ameitoa wakati wa mkutano wa Global Gateway Forum ambao rais Kagame pia anahudhuria jijini Brussels nchini Ubelgiji.

Tshisekedi, alizungumza baada ya Kagame kuzungumza kwenye mkutano huo wa uwekezaji ulioandaliwa na Umoja wa Ulaya jijini Brussels.

“Natangaza kwenye mkutano huu na kwa dunia nzima kufikisha mkono wangu kwako rais ilitufanye amani.” Alisema Rais Tshisekedi.

“Hili linakuhitaji wewe kuwaagiza waasi wa M23 ambao nchi yako inawaunga mkono kuacha kuchochea mzozo huu ambao umesababisha vifo vya watu wengi” Alisisitiza Rais wa DRC.

“Wacha tuwe na ujasiri wa kujiangalia na kujiuliza tatizo liko wapo na kuchukua uamuzi unaostahili kwa ajili ya watu wetu” aliongeza Rais wa DRC.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi kuacha kuwaunga mkono waasi mashariki ya nchi yake na kwamba washirikiane kwa ajili ya amani.

Kagame hakuwa amezungumzia moja kwa moja mzozo wa mashariki ya DRC wakati alipopewa nafasi ya kuzunguza.

Alisikika tu akigusia hotuba ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye wakati akiongea alisema alihisi kupata nguvu ya kutegeneza amani baada ya kuwaona wenzake wa DRC na Rwanda.

 “Baadhi yetu tulihisi hivyo. Tulihisi kupata nguvu za kibiashara, uwekezaji na amani.” alisema Kagame.

Eneo la mashariki ya DRC, mpaka na Rwanda limekuwa likikabiliwa na utovu wa usalama kwa zaidi ya miongo mitatu, makundi yenye silaha yakiwashambulia raia.

Kundi la waasi wa M23 ambalo lilianzisha uasi mpya mwishoni mwa mwaka wa 2021 linaungwa mkono na wanajeshi wa Rwanda mashariki ya Congo, uasi ambao umezua mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Mapigano mapya yalizuka tena mapema mwaka huu ambapo  waasi wa M23 walichukua udhibiti wa Miji muhimu ya Bukavu na Goma likitangaza utawala wake kwenye Miji hiyo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, tangu mwezi Januari mwaka huu, maelfu ya watu wamefariki kwenye mapigano wakati mamia kwa maelfu yaw engine wakitoroka makazi yao.

Comments are closed.