Mke wa Rais wa Brazil aambukizwa Coronavirus

14,617

Mkewe Rais wa Brazil Jiar Bolsonaro amepatikana na virusi vya corona, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya ikulu

Habari kuhusu kuambukizwa kwake yanajiri siku chache tu baada Rais huyo kupona

Virusi vya corona vimetikisa nchi ya Brazil kwa mara nyingine, wakati huu mkewe Jiar Bolsonaro rais wa nchi hiyo akitangazwa kuugua virusi hivyo hatari.

Ripoti kuhusu kuambukizwa  kwa Michelle Bolsonaro inajiri siku chache tu baada ya mumewe aliyeammbukizwa vile vile kutangaza kuwa amepata afueni.

Kulingana na taarifa kutoka ikulu, licha ya kuambukizwa virusi hivyo, Michelle yuko katika hali imara na kuwa madaktari wa ikulu wanafanya kila nia kuhakikisha anapona upesi.

‘’ Hali yake iko imara na tunafuatilia kila kitu kwa karibu,’’idara ya habari na mawasiliano katika ikulu ilitaarifu.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, Michelle alipatikana na virusi vya corona Julai 30, siku moja tu baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara akiandamana na mumewe.

Akihudhuria mkutano huo, Michelle na mumewe walionekana wakiwa wamevalia barakoa kama njia ya kujikinga.

Comments are closed.