Ronaldo kuijunga na Messi Barcelona

13,101

Juventus wameipa Barcelona ofa ya kumsajili kiungo wa Ureno Cristiano Ronaldo, usajili ambao huenda ukawa wa ubishi mkubwa duniani endapo utafanyika kutokana na usbishi uliopo kati ya wafuasi wa Ronaldo na Messi.

 Kwa mjibu wa mwanhabari wa michezo wa uhispania  Guillem Balague. Ni Juventus wanajaribu kila wawezalo kumdondosha Ronaldo kwa club yoyote ile ambayo itakuwa na uwezo wa kulipa mishahara yake .

 Kwa sasa mjiniTurin Ronaldo anamkataba wa euro million 28 kila mwaka fedha ambazo kwa sasa Juventus wanapitia wakati mgumu kumlipa ronaldo baada ya kumaliza misimu miwili naye.

Barcelona pia wa sasa wanapitia wakati mgumu wa kifedha na ni kati ya vilabu vilivyoathirika zaidi kote duniani.

Juventus wana mkufunzi mpya Andrea Pirlo ambaye anapania kujenga kikosi chake kipya na huenda Ronaldo, Aaron Ramsey na Paul Dybala ni kati ya wachezaji watakao uzwa kutoa nafasi ya kuwasajili wachezaji zaidi.

Mwaka wa 2018 Ronaldo alijiunga na Juventus akitokea Real Madrid na kuikata ofa ya kwanza iliokuwa imetolewa na PSG ya Ufaransa.

Comments are closed.