Aliyefanya mashambulizi kwenye misikiti New Zealand amekiri kuwa alipanga kuua watu wengi zaidi

13,130
Flowers in Christchurch after the shootings in March 2019

Mwanaume aliyeua watu 51 katika misikiti miwili nchini New Zealand mwaka 2019 alikuwa na mipango ya kulenga msikiti mwingine wa tatu.

Brenton Tarrant pia alipanga kuchoma moto misikiti, akitaka ”kusababisha athari kubwa inavyowezekana.”

Raia huyo wa Australia ambaye amekiri kuwa na hatia ya makosa 51 ya mauaji, na 40 ya kujaribu kuua na tuhuma za ugaidi.

Tarrant, 29, anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani, inawezekana bila msamaha – hukumu ambayo haijawahi hapo kabla kutolewa nchini New Zealand.

Alikabiliwa na walionusurika na mashambulio hayo na ndugu walioathirika alipowasili mahakamani Jumatatu.

”Umejipa mwenyewe mamlaka ya kuondoa roho za watu 51 wasio na hatia, kosa kubwa machoni pako- ni kuwa waislamu,” alisema Maysoon Salama, ambaye kijana wake Atta Elayyan aliuawa.

Mashambulizi ambayo kwa sehemu mtu huyo mwenye silaha aliyarusha moja kwa moja mtandaoni, alionekana wazi akifyatua risasi kwenye misikiti miwili mjini Christchurch tarehe 15 mwezi Machi mwaka jana.

Kwanza aliendesha gari mpaka kwenye msikiti wa Al Noor, akawashambulia watu waliokuwa wakisali ibada ya Ijumaa.

Kisha akaelekea umbali wa kilomita 5 kwenye msikiti wa Linwood na kuua watu zaidi.

Shambulio hilo lilishitua ulimwengu hatua iliyofanya New Zealand kufanyia mabadiliko sheria ya silaha.

Relatives of victims arrive at Christchurch High Court, 24 August 2020

Shambulio lilitokeya aje?

Kesi ya hukumu, ambayo itakwenda mpaka siku nne ilianza asubuhi ya Jumatatu mjini Christchurch.

Masharti ya kukabili Covid-19 yamefanya vyumba vya mahakama kuwa vitupu. Mamia ya watu watafuatilia kesi hiyo kwa njia ya video kutoka kwenye vyumba vingine vya mahakama mjini humo ikiwa ni utekelezaji wa amri ya kutochangamana.

Akiwa na mavazi ya kijivu, sare ya gerezani na kuzungukwa na maafisa wa polisi, mtuhumiwa alisalia kimya, mara kadhaa akiangaza ndani ya chumba hicho ambacho walionusurika na ndugu wa aliopoteza maisha walikuwa wamekaa.

Brenton Tarrant during sentencing at the High Court in Christchurch

Mwendesha mashtaka Barnaby Hawes aliiambia mahakama kuwa mtu huyo aliyekuwa na silaha alianza kutengeneza mpango miaka kadhaa kabla, na nia yake ilikua ”kusababisha vifo vingi iwezekanavyo.”

Alikusanya taarifa kuhusu misikiti nchini New Zealand- akiwa na nia ya kuwalenga katika muda wataokuwa na pilika nyingi.

Miezi kadhaa kabla ya shambulio, alisafiri mpaka Christchurch na kurusha drone kuelekea kwenye eneo alilolilenga, msikiti wa Al Noor.

Pia alipanga kulenga msikiti wa Ashburton baada ya Al Noor na kituo cha kiislamu cha Linwood, lakini alikamatwa alipokuwa akielekea kwenye msikiti wa tatu.

Siku hiyo ya shambulizi, aliwafyatulia watu risasi mtaani walipokuwa wakijaribu kukimbia kutoka kwenye msikiti wa Al Noor, mahakama ilieleza.

Akiwemo mtu mmoja kwa jina Ansi Alibava, ambaye aligongwa alipokuwa akiondoka msikitini hapo.

Alipokuwa akiendesha gari kuelekea kwenye kituo cha kiislamu, alisimama na kuwafyatulia risasi wanaume wenye asili ya Afrika ambao walifanikiwa kukimbia. Kisha alielekeza bunduki kwa mtu mwenye asili ya weupe, mahakama ilisikika ikisema, lakini ”alitabasamu kisha aliondosha gari”.

Aliwaambia polisi baada ya kukamatwa kuwa mipango yake ilikuwa kuchoma moto misikiti baada ya shambulio, na kuwa anatamani angekuwa amefanya hivyo.

Tarrant anajisimamia mwenyewe mahakamani. Awali alikana mashtaka dhidi yake.

Anakabiliwa na kifungo cha chini cha miaka 17, lakini jaji Cameron Mander, Jaji wa mahakama ya juu, ana mamlaka ya kumhukumu kifungo cha maisha bila msamaha, hukumu ambayo haijawahi kutangazwa New Zealand.

Alisema aliona. ”Chuki machoni mwa gaidi aliyepotoshwa” alipokuwa amesimama kwenye membari, alisema Tarrant: ”Chuki yako haina sababu.”

Mtoto wa Ashraf Ali aliyeathirika, amesema bado anateswa na tukio hilo: ”Nina kumbukumbu, kuona miili ikiwa imenizunguka. Damu imetapakaa kila mahali.”

Waziri Mkuu Jacinda Ardern alisema itakuwa wiki ngumu kwa walioathirika na familia za waliopoteza maisha.

”Sifikirii kuna kingine ninachoweza kusema kitaondoa machungu ambayo yatakuwepo kipindi hicho,” alisema juma lililopita.

Chini ya mwezi mmoja baada ya mashambulizi, bunge la New Zealand ilipiga kura 119 kwa 1 kuhusu mabadiliko ya matumizi ya silaha pia kuzuia vipuri ambavyo vinaweza kutengeneza silaha zilizopigwa marufuku.

Serikali imetangaza kulipa fidia wamiliki wa silaha ambazo kwa sasa zimepigwa marufuku ambapo watazichukua kwa mfumo wa kuzinunua kutoka kwa wamiliki.

Comments are closed.